29 Desemba 2025 - 15:30
Pendekezo la utaratibu mpya wa kumchagua Rais wa Iraq kutoka kwa Masoud Barzani

Masoud Barzani amewasilisha utaratibu mpya wa kumchagua Rais wa Iraq, kwa lengo la kuimarisha mshikamano wa Wakurdi na kuimarisha nafasi yao katika wadhifa huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Masoud Barzani, rais wa Chama cha Kidemokrasia cha Kurdistan (KDP), leo Jumatatu ametangaza pendekezo la utaratibu mpya wa kumchagua Rais wa Iraq. Utaratibu huo unalenga kuimarisha nafasi ya Wakurdi katika urais wa nchi na kufanikisha mwafaka miongoni mwa mikondo yote ya kisiasa ya Kurdistan.


Katika taarifa yake, Barzani alisisitiza akisema:
“Wadhifa wa Rais wa Iraq unapaswa kuthibitishwa kama ni sehemu ya haki ya Wakurdi, na rais atakayechaguliwa anapaswa kuwa mwakilishi wa kweli wa wananchi wa Kurdistan. Kwa hiyo, ni lazima njia ya uchaguzi ibadilishwe, na hakuna mkondo au chama kinachopaswa kuuchukulia wadhifa huu kama mali binafsi au ya kipekee.”


Barzani alieleza kuwa utaratibu huo mpya unajumuisha chaguzi kadhaa, zikiwemo:
Kuteuliwa kwa mtu mmoja na Bunge la Kurdistan kama mwakilishi wa Wakurdi kwa ajili ya kushika wadhifa wa Rais wa Iraq,
Kufikiwa kwa makubaliano ya pamoja ya mikondo yote ya kisiasa ya Kurdistan juu ya mgombea mmoja maalumu,
Au kuchaguliwa kwa mtu na wabunge na makundi ya Kibunge ya Wakurdi katika Bunge la Iraq.


Aidha, Barzani alibainisha kuwa rais atakayechaguliwa si lazima atoke katika Chama cha Kidemokrasia cha Kurdistan au Umoja wa Kizalendo wa Kurdistan (PUK), bali anaweza kuwa kutoka mkondo mwingine wa kisiasa au hata kuwa mtu huru, mradi tu apate mwafaka wa Wakurdi na aweze kwa ufanisi kuwawakilisha wananchi wa Kurdistan katika nafasi ya urais wa Iraq.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha